1. Umri
Watu wa rika zote WANAWEZA kuambukizwa na virusi vya Korona.Wazee, na watu ambao wako katika hali ya matibabu ( kama kisukari, magonjwa ya moyo, pumu) wanakuwa katika hatari zaidi ya kuwa wagonjwa zaidi wakipata hichi kirusi.
2. Hali ya Hewa ya Baridi
Hali ya baridi na barafu HAVIWEZI kuuwa kirusi
3. Hali ya Hewa ya Joto
Kirusi cha Korona KINAWEZA kusambazwa kwenye hali ya joto na unyevunyevu
4. Kusambazwa na mbu
Kirusi cha korona HAKIWEZI kusambazwa kwa njia ya mbu.
5. Kuoga na Maji ya moto
Kuoga na maji moto HAKUZUII kirusi cha korona
6. Vipima joto
Vipima joto VINAWEZA kujuza endapo mtu ana homa lakini SIO kujua kama mtu anavirusi vya korona
7. Kujipuliza klolini au kileo
Kujipulizia klolini au kileo mwili mzima HAIZUII kuuwa virusi ambavyo vimeshaingia mwilini
8. Kunawa pua na maji ya saline inakupa kinga
HAKUNA ushahidi ya kwamba kunawa pua na maji ya saline mara kwa mara hukinga watu na maambukizi ya kirusi cha korona.
9. Chanjo dhidi ya pumu kukukinga dhidi ya Korona
Chanjo dhidi ya pumu, kama chanjo ya pneumococcal na Haemophilus influenza type b ( Hib), HAVIWEZI kukukinga dhidi ya kirusi cha korona.
10. Kunywa dawa za kuuwa bakteria
Dawa za kuuwa bakteria HAZIFANYI KAZI dhidi ya kuuwa virusi, zinafanya kazi ya kuuwa bakteria tu.
Mpaka leo, HAKUNA dawa maalum iliyopendekezwa ya kuzuia au kutibu kirusi cha korona.
Pata ukweli zaidi kwenye tovuti ya WHO: https://www.who.int/emergencies/diseases/novel-coronavirus-2019/advice-for-public/myth-busters