Mtu anaweza kupata ugonjwa wa COVID-19 kutoka kwa watu wenye kirusi.

Ugonjwa unaweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia matone madogo kutoka puani au mdomoni mwa mgonjwa wa COVID-19 anapokohoa au kutoa hewa.

Matone haya hutua kwenye vifaa/vitu na maeneo yanayomzunguka binadamu.

Watu wengine hupata ugonjwa wa COVID-19 kwa kugusa vitu hivi, kisha kujigusa machoni, puani au mdomoni.

Pia mtu anaweza kupata COVID-19 ikiwa anavuta matone kutoka kwa mtu aliye na COVID-19 anayekohoa au kutoa hewa nje. Hii ndio sababu ni muhimu kukaa mbali na mtu ambaye ni mgonjwa zaidi ya mita 1 (miguu 3).

WHO ikiwa inakagua utafiti unaoendelea juu ya njia ambazo COVID-19 imeenea na itaendelea kutoa matokeo mapya.