Dalili za kawaida za ugonjwa wa COVID-19 ni:
- Homa
- Uchovu
- Kikohozi kikavu.
- Baadhi ya wagonjwa wanaweza kupata maumivu, msuguano wa pua, kutokwa kwa majimaji puani, vodonda vya koo au kuharisha.
- Dalili hizi huanza polepole. Baadhi ya watu wanapata maambukizi bila kuonesha dalili zozote za ugonjwa.
- Watu wengi (takribani 80%) wanapona kutokana na ugonjwa huu bila ya matibabu maalum. Takribani katika kila watu 6 wenye ugonjwa wa COVID-19 mtu 1 huwa mgonjwa sana na kupelekea kupumua kwa shida.
- Wazee na wale wenye shida za kimatibabu kama vile shinikizo la damu, matatizo ya moyo au ugonjwa wa kisukari wana uwezekano wa kupata ugonjwa kwa dalili mbaya.
- Watu wenye homa, kikohozi na ugumu wa kupumua wanapaswa kupata matibabu.