Kama hivi karibuni ( siku 14 zilizopita) umetembelea maeneo ambayo COVID-19 imesambaa, fuata muongozo uliotolewa kwenye swali la 15. ( Nini naweza kufanya ili kujikinga na kuzuia maambukizi?) kisha fanya yafuatayo:
- Jitenge kwa kukaa nyumbani mpaka upone hii ni kama umeanza kutojisikia vizuri,hata kama dalili ni za kiasi kama kichwa kuuma, homa ya chini ( nyuzi joto 37.3 C au zaidi ) na kuvuja kwa pua.
- Kama inawezekana kuwa na mtu wa kukuletea mahitaji yako au ukitoka nje kununua chakula, basi vaa barakoa ( mask) kuzuia kuwaambukiza wengine. Kwanini? – Kuzuia kukutana na watu wengine na kwenda katika vituo vya afya vitafanya vituo hivi kufanya kazi kwa ufanisi na kuwasaidia kujilinda mwenyewe na wengine dhidi ya COVID-19 na virusi vingine.
- Ukipata homa, kikohozi na shida ya kupumua, fata ushauri wa kiafya zaidi inawezekana kuwa na maambukizi kwenye njia ya hewa au matatizo mengine makubwa zaidi. Piga simu na kuwajulisha watoa huduma ya afya juu ya safari zako za karibuni au mkutaniko na wasafiri. Kwanini? – Kupiga simu hii itawasaidia watoa huduma kukuelekeza kituo sahihi cha afya karibu na wewe. Hii pia huzuia kusambaza COVID-19 na virusi vingine.