Virusi vya korona ni familia kubwa ya virusi ambayo ni vya kawaida katika wanyama. Wakati mwingine, watu huambukizwa na virusi hivi ambavyo vinaweza kuenea kwa watu wengine. Kwa mfano, SARS-CoV ilihusishwa na paka na MERS-CoV husambazwa na ngamia. Uwezekano wa wanyama kuwa chanzo cha COVID-19 bado haujathibitishwa

Ili kujikinga, kama vile wakati wa kutembelea masoko ya wanyama hai, epuka kugusana moja kwa moja na wanyama pamoja na mazingira yao. Hakikisha mazoea mazuri ya usalama wa chakula wakati wote. Hifadhi nyama mbichi, maziwa au sehemu za wanyama kwa uangalifu ili kuzuia uchafuzi wa vyakula visivyopikwa na epuka kula bidhaa mbichi za wanyama au ambazo hazijaiva vizuri katika kupikwa.