1. Zingatia habari za hivi karibuni juu ya milipuko ya COVID-19, inayopatikana kwenye Shirika la Afya Duniani (WHO) na kupitia mamlaka yako ya kitaifa ya afya. Nchi nyingi duniani kote zimesharipoti kesi za milipuko ya COVID-19. Nchini China na baadhi ya nchi zingine zimefanikiwa kupunguza au kuzuia milipuko yao. Walakini, hali hiyo haitabiriki hivyo tembelelea mara kwa mara kwa habari mpya zaidi. Unaweza kupunguza nafasi ya kuambukizwa au kueneza COVID-19 kwa kuchukua tahadhari rahisi

2. Safisha mikono yako mara kwa mara kwa kutumia vitakasa au osha kwa sabuni na maji.

Kwanini? – Kuosha mikono yako kwa sabuni na maji au kutumia vitakasa huua virusi ambavyo vinaweza kuwepo mikononi mwako

3. Kaa umbali wa angalau mita 1 (miguu 3) kati yako na mtu yeyote anayekohoa au kupiga chafya.

Kwa nini? Wakati mtu anakohoa au kupiga chafya hunyunyiza matone ya kioevu kutoka puani au mdomoni ambayo yanaweza kuwa na virusi. Ikiwa upo karibu naye Zaidi, unaweza kuvuta matone pamoja na virusi vya COVID-19 ikiwa mtu anayekohoa ana ugonjwa.

4. Epuka kugusa macho, pua na mdomo

Kwa nini? Mikono hugusa sehemu mbalimbali na inaweza kuchukua virusi. Mara ikichukua virusi, inaweza kupeleka virusi hivyo kwenye macho yako, pua au mdomo. Baada ya hapo, virusi vinaweza kuingia ndani ya mwili wako na vinaweza kukufanya uwe mgonjwa.

5. Hakikisha wewe, pamoja na watu wanaokuzunguka, mnafuata usafi mzuri wa kupumua. Hii inamaanisha kufunika mdomo wako na pua kwa kiwiko cha mkono wako au tishu wakati unapokohoa au kupiga chafya. Kisha tupa tishu zilizotumika mara moja.

Kwa nini? Matone hueneza virusi. Kwa kufuata usafi mzuri wa kupumua unalinda watu wanaokuzunguka kujilinda na virusi kama vile homa, mafua na COVID-19

6. Kaa nyumbani ikiwa unajisikia vibaya. Ikiwa una homa, kukohoa na kupumua kwa shida,pigi simu mapema ili kupata matibabu. Fuata maagizo ya mamlaka ya afya ya eneo lako.

Kwa nini? Mamlaka ya kitaifa na ya ndani zinapata habari mpya kuhusu haliya sasa katika eneo lako. Kupigia simu mapema itaruhusu mtoaji wako wa huduma ya afya kukuelekeza haraka katika kituo cha afya kinachofaa. Hii pia itakulinda na kusaidia kuzuia kuenea kwa virusi na maambukizi mengine.

7. Fuatilia habari mpya za hivi karibuni za COVID-19 (miji au maeneo ya ndani ambayo COVID-19 inaenea sana). Ikiwezekana, epuka kusafiri kwenda maeneo – haswa ikiwa wewe ni mzee au una ugonjwa wa kisukari, moyo au mapafu.

Kwa nini? Una nafasi ya juu ya kupata maambukizi ya COVID-19 katika moja ya maeneo haya.